Karibu Katika mtandao wa Shirika la Cartoon Forum Tanzania, katika mtandao huu utapata kujua mambo mengi kuhusiana na Shirika hili pia kupata matukio, picha na katuni mbalimbali zenye kuelimisha. Hivyo ni nafasi yako kujifunza na pia kutoa maoni yako, KARIBU SANA...

Thursday, December 21, 2017

Rushwa ya ngono kwa wasichana wa kazi huzalisha madanguro 

Na Adam Malinda, Kwa hisani ya Cartoon Forum Tanzania.

TUNAPOZUNGUMZIA rushwa, zipo za aina mbalimbali katika jamii, zote zinaleta athari kubwa kiuchumi na kijamii, lakini pia huleta athari katika vizazi vya sasa na vijavyo, rushwa hii isipodhibitiwa italitokomeza taifa na kupoteza utu wa mwanamke.

Monday, December 11, 2017




Washiriki wa Mkutano wa kupiga vita Rushwa
ya ngono wakionesha mabango yenye ujumbe wa vita hiyo.









Rushwa ya ngono sehemu za kazi huondoa heshima ya utu, hupunguza tija.

Na Adam Malinda,
Kwa Hisani ya Cartoon Forum Tanzania.


RUSHWA ya ngono ni aina mojawapo ya rushwa ambazo zimeleta athari kubwa katika  Jamii hasa katika maeneo ya kazi, baadhi wameshindwa kuichukia kwa kutokujua, wengine kwa kutofahamu namna inavyodhalilisha utu wa mtu, lakini baadhi yao kwa kutofahamu namna ya kupambana na changamoto inayowakabili ambayo ni kujiamini na kusimamia kile wanachokiamini.